Hatimaye FUTURE aweka hadharani Jinsia ya Mtoto wake Mtarajiwa

RAPPER FUTURE ni moja kati ya Rappers Nchini Marekani ambaye ana idadi kubwa kidogo ya watoto na hasa kila mmoja akiwa anatoka kwa mama yake, yaani sio watoto wa mama mmoja.

Future ambaye alishutumiwa sana na bado anaendelea kushutumiwa sana kuhusu kutokutulia katika mahusiano yake ambayo anayaanzisha, amewahi pia kuwa na mahusiano na Msanii wa Kike wa R&B/POP, CIARA PRINCESS HARRIS maarufu kama “Ciara” na kufanikiwa kupata mtoto mmoja, lakini mahusiano yao hayakudumu kama walivyotatarajia baada ya Future “kuchepuka”

Ukiachilia mbali suala hilo, Hatimaye Rapper huyo ambaye ni Hitmaker wa “TURN OFF THE LIGHT” pamoja na mpenzi wake JOIE CHAVIS wameweka hadharani jinsia ya mtoto wao ambaye atafuatia na kukamislisha idadi ya jumla watoto 6.

Katika sherehe ambayo iliandaliwa nyumbani kwake na Mpenzi wake huyo, Wawili hao wameweka wazi kuwa mtoto ambaye wanatarajia kumpata ni jinsia ya kiume.

JOIE CHAVIS ambaye awali alikuwa ni Girlfriend wa Rapper BOW WOW, ndiye alikuwa mtu wa kwanza kabisa kuvujisha taarifa za kuwa na ujauziti na Rapper huyo wa Mkwaju wa MASK OFF, ingawa awali haikuwa makubaliano yao kufanya hivyo

TUNAWATAKIA KILA LA KHERI katika kupata mtoto mwingine

Facebook Comments

Related posts