MAMA AMUUA MWANAE KWA KIPIGO AKIMTUHUMU KUIBA MAEMBE KWA JIRANI,

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia mwanamke mmoja aitwaye RAHEL MATALAKA, miaka 41, mkazi wa kijiji cha lugenge, kwa tuhuma za kumpiga hadi kumuua mtoto wake wa kiume aitwaye MALIATABU CONSTANTINE, miaka 10, mwanafunza wa darasa la pili shule ya msingi Ikeleg,Wilayani Misungwi.

Tukio hilo la mauaji limetokea tarehe 03.11.2018 majira ya 1:00 jion, hii ni baada ya mama wa marehemu kupokea malalamiko kuwa mtoto wake alikua akiangusha na kuiba maembe kwa jirani. Ndipo mtuhumiwa alipatwa na hasira na kumpiga mtoto kwa kutumia fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake hali iliyopelekea mtoto kupoteza fahamu na baadae kufariki dunia.

Mtuhumiwa alipoona mtoto amepoteza maisha alimchukua na kumtundika juu ya mwembe kwa kutumia kipande cha khanga ili apoteze ushahidi ili baadae ionekane kuwa amejinyonga. Ndipo majirani walipoona tukio hilo walitoa taarifa kituo cha Polisi. Aidha baada ya polisi kupata taarifa hizo tulifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa.

Kamanda wa police Mkoa wa Mwanza Jonathan Shanna amethibitisha kutoka kwa tukio hilo na kusema
Polisi wanaendelea na mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani,Huku Mwili wa marehemu tayari umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.

Facebook Comments

Related posts