Alliance Nyamagana kazi wanaiweza.

Kikosi cha Alliance kimenifakiwa kushinda Mchezo wake wapili mfululizo Katika uwanja wa wake wa Nyamagana Baada ya leo kuicharaza Mtibwa 1-0 Katika mchezo wa Ligi kuu soka Tanzania Bara.

Hii ni alama ya 7 sasa anaikusanya kocha wa muda wa Alliance “Dadi” ambaye mechi yake ya kwanza alitoka sare na Costal Union, mechi ya pili akamfunga Singida United na ya tatu ya leo akiitafuna miwa ya Mtibwa.

Goli pekee la Alliance Katika mchezo wa leo limefungwa na nyota machachari Dickson Ambundo Katika dakika ya 53.

“Naamini Katika Philosophy na ya kwangu imefanya kazi” maneno ya Dadi Baada ya kupata ushindi Leo.

Facebook Comments

Related posts