Lukaku kuikosa mechi ya kulipiza kisasi Leo.

Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku ataikosa mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya leo pale Allianz Stadium dhidi ya Juventus baada ya kuumia.

Jose Mourinho pia alithibitisha kwamba Straika huyo yupo shakani kuikabili Manchester City siku ya Jumapili.

Lukaku hakufanya mazoezi siku ya Jumanne kujiandaa na mechi ya leo ya Jumatano dhidi ya Juventus na aliikosa mechi ya Jumamosi dhidi ya Bournemouth.

United inasfiri mpaka pale Turin leo wakihitaji kulipiza kisasi Baada ya kuchapwa goli moja kwenye Mchezo uliopita dhidi ya Juve pale Old Trafford.

Facebook Comments

Related posts