U.S.A: Chama cha rais Donald Trump, Republicans kimepoteza wingi katika bunge la Congress:

Chama cha rais Donald Trump, Republicans kimepoteza wingi katika bunge la Congress hali ambayo itafanya muda uliosalia wa urais wa Trump kupitia wakati mgumu zaidi.
Republicans pia wamepoteza viti saba vya Ugavana mpaka sasa. Hata hivyo chama hicho kimefanikiwa kubaki na wingi katika bunge la Seneti.
Kwenye uchaguzi wa bunge la Congress, mpaka sasa majimbo 412 yametangaza matokeo. Democrats wanaongoza kwa viti 219 huku Republicans wakifuatia na viti 193.
#chanzobbcswahili

Facebook Comments

Related posts