Watakatifu waanza kwa kufyekelea mbali uongozi.

Southampton wamemfukuza kazi Les Reed ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wao wakitoa sababu kwamba wanataka muongozo mpya ili kubadilisha matokeo mabaya.

Maamuzi hayo yamekuja baada ya mtiririko wa mechi saba mfululizo bila ya ushindi na klabu ipo pointi mbili tu mbele ya washika mkia Fulham.

Hiyo imekuja pia baada ya taarifa kwamba Southampton wanataka kumfukuza kazi kocha Mark Hughes endapo atashindwa kuifunga Watford wikiendi hii.

Facebook Comments

Related posts