Vita ya Dernmak na Wales Kesho Bale yutayari kuwanyoosha.

Kocha wa timu ya taifa ya Wales Ryan Giggs ameweka wazi Kwamba Gareth Bale yuko fiti kuivaa Denmark kwenye michuano ya UEFA NATIONS LIGUE mchezo wa kamua hatima ya Kundi lao Kesho.

Bale alikuwa matatani kuwepo katika mchezo huo wa Kesho kutokana na jeraha alilolipata siku ya jumapili wakati Madrid ikiichapa 4-2 Celta Vigo.

Bale (29) alijunga na kikosi cha Wales leo asubuhi na Giggs ana matumaini yakumtumia katika mchezo wa Ijumaa hii dhidi ya Denmark utakaofanyika mjini Cardiff.

“Anaonekana yupo sawa wiki hii na yupo tayari” maneno ya Giggs akimzungumia Bale.

Facebook Comments

Related posts