Rooney amuunga mkono Kane kuivunja rekodi yake.

Harry Kane ana nafasi ya kuwa mfungaji bora wa taifa la England na hilo ni kwa mujibu wa Wayne Rooney.

Rooney amempa moyo Nahodha huyo wa England Kwamba anaweza kufikia magoli 53 ambayo ameyafunga yeye akiwa na taifa hilo.

Rooney mshambuliaji wa zamani wa Everton na Manchester United amestaafu rasmi kulitumikia taifa la England baada ya kucheza mechi ya mwisho Alhamis usiku katika uwanja wa Wembley England ikishinda 3-0 dhidi ya Marekani.

Baada ya Rooney kustaafu akiwa Ndio kinara wa magoli katika taifa la England akicheka na nyavu mara 53 anaamini mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane ambaye kashafikisha magoli 19 ataivunja rekodi yake.

Rooney yeye alivunja rekodi ya kuwa kinara wa magoli katika taifa la England rekodi ambayo kwa muda mrefu ilikuwa ikishikiliwa na Sir Bob Charlton ambaye enzi za uchezaji wake alifunga magoli 49.

 

Facebook Comments

Related posts