Baada ya Kipigo pale Maseru Amunike ajishusha.

Kocha wa Stars Mnigeria Emmanuel Amunike amewaomba radhi Watanzania kwa matokeo ya kipigo cha timu ya Taifa Stars cha bao 1-0 toka kwa Lesotho katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika AFCON uliopigwa mjini Maseru, Lesotho.

Matokeo hayo yameiweka njia panda Stars katika kufuzu kwa fainali hizo zitakazofanyika mwakani nchini Cameroon.

Tanzania ipo Kundi L katika michuano hii kwa matokeo haya inalingana alama na Lesotho wenye alama tano pia, huku Cape Verde nao wakiwa na alama 4 Uganda akiwa ameshafuzu na alama zake 13.

Stars sasa inahitaji Ushindi mchezo wao wa mwisho dhidi ya Uganda utakaopigwa mwakani hapa Tanzania huku wakiombea sare au Cape Verde imcharaze Lesotho mechi yao ya mwisho.

Facebook Comments

Related posts