ABAKWA NA WANAUME WAWILI NJIANI AKIELEKEA KUJIFUNGUA

 

Mwanamke mmoja mjamzito ameripotiwa kubakwa na wanaume wawili mbele ya watoto wake akiwa njian kwenda hospitali kujifungua.

Mjamzito huyo kutoka mtaa wa Huruma jijini nairobi siku ya tukio akiwa na mwanaye walikutana na wanaume hao waliowachukua kwa nguvu hadi vichakani na kumbaka bila kujali hali yake mbele ya mwanaye.

Wabakaji hao walidaiwa kumtishia mama huyo kumuua endapo atatoa taarifa polisi.

Tayari maafisa wa polisi wamefanikiwa kumtambua mmoja wa washukiwa hao wa ubakaji aitwaye Kamau au kwa jina la utani Kamare ambaye anaishi na mjombake katika eneo la Mlango Kubwa karibu na mtaa wa Huruma.

Mama huyo aliripotiwa kupata msaada kutoka kwa dereva wa pikipiki aliyempeleka hospitalini akiwa mahututi.

Facebook Comments

Related posts