APONZWA NA KITABU CHA NGONO ,SASA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA MIAKA KUMI GEREZANI

Mwandishi mmoja wa vitabu nchini Uchina amefungwa miaka 10 jela kwa kuandika na kuuza kitabu chenye maudhui ya ngono ya wapenzi wa jinsia moja.

Mwandishi huyo mwanamke afahamikaye kwa jina la Liu, alihukumiwa kifungo hicho na na mahakama ya jimbo la Anhui mwezi uliopita kwa kuuza “maudhui machafu”.

Jina la kitabu hicho ni “Occupation”, lenye maana ya kazi kwa kiswahili na kimebeba maudhui ya “tabia ya ngono ya wapenzi wa jinsia noja wa kiume…pamoja na aina za kupotosha za ngono na kwenda kinyume na jamii.”

Kwa mujibu wa shirika la habari la Beijing News, bi Liu – ambaye anafahamika zaidi mtandaoni kama kama Tian Yi – tayari amaeshakata rufaa dhidi ya adhabu hiyo.

Kutengeneza na kusambaza maudhui ya ngono ni kinyume cha sheria nchini Uchina.

Hukumu hiyo ilitolewa Oktoba 31, lakini habari hiyo imeripotiwa na vyombo vya habari hivi karibuni.

Facebook Comments

Related posts