MBARONI KWA KULEWESHA WANAUME NA KUWAIBIA

 

Polisi nchini Kenya wamefanikiwa kuwatia nguvuni wanawake wawili wauza milii kwa kosa la kuwachaganyia dawa za kulevya wateja wao na kuwaibia.

Wanawake hao Mary Nyaguthii Mathari na Mary Nyamwea Gathiaka walikamatwa Ijumaa, Novemba 16, na walipatikana na dawa kadha zinazoaminiwa kutumiwa kuwalevywa wateja wao katika vilabu vya burudani.

Mbali na dawa hizo walikamatwa na kadi za simu na za kutolea pesa.

“Makechero waliotumia ripoti za kijasusi waliwakamata wanawake wawili; Mary Nyaguthii Mathari na Mary Nyamwea Gathiaka mjini Thika kwa madai ya kuwalevywa wateja wao kabla ya kuwaibia. Tembe kadhaa za Stilnox zinazotumiwa kuwalevywa watu na kadi mbalimbali za simu zilipatikana,” ujumbe wa Twitter kutoka kwa DCI ulisema.

“Kadi hizo zilizosajiliwa kwa kutumia majina mbalimbali zinaaminiwa kutumika kutolea pesa kutoka kwa akaunti za walioleweshwa na dawa zao” ripoti hiyo ilisema.

Katika siku za karibuni, watu kadhaa wamekamatwa kwa visa vya aiana hiyo. Jumanne, Oktoba 9, makachero walimkamata Everline Wambui Mutura aliyemlaghai Patrick Mwaura Kungu kutoka Parklands na kumpeleka Ngara na kisha akampora kadi ya ATM na kitambulisho.

Facebook Comments

Related posts