Neymar wewe na Ramosi kwani mna ugomvi?.

Taarifa zinasema kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Brazili na Klabu ya PSG ya pale Ufaransa Neymar Jr anahitaji beki wa Real Madrid Sergio Ramos aondeke ndipo ajiunge na Klabu hiyo Tajiri wa Jiji la Madrid.

Sasa swali ni Kwamba inawezekana Ramos akawa kikwazo cha Neymar Jr kujiunga na Real Madrid ambayo inamuhitaji kwa muda mrefu?

Taarifa kutoka Don Balon zinadai mbrazili huyo hayuko tayari kucheza na Nyota huyo kihispania na hata weza kujiunga na Madrid endapo Ramos yupo kwenye timu.

Makisio ya Chanzo cha Neymar kutohitaji kucheza na Ramosi timu moja. 

Ramos alishawahi kumkaribisha Neymar kujiunga na Klabu ya Real Madrid ilikuwa ni mwishoni mwa mwaka 2017 wakati huo Neymar kajiunga na Klabu ya PSG akitokea Barcelona.

“Napenda kucheza na mchezaji bora ambaye analeta tofauti na Neymar ni miongoni mwao” Ramosi akimzungumia Neymar.

“Ni rahisi kuhama kutoka PSG kuja Real Madrid kuliko kutoka Barcelona moja kwa moja” aliongezea Ramosi.

Lakini Ramosi alimtania Neymar kipindi hicho.

“Tunacho paswa kukubaliana naye Nikuhusu siku ya kuzaliwa ya Dada yake [akacheka] ”

Inaonekana kama Neymar huo utani hajapenda na huwenda inakuwa kikwazo kucheza na aliyemtaniaga.

Mwaka 2016 Neymar akiwa Barca aliwahi kulalamikiwa kwa kucheza chini ya kiwango Lakini baada ya kupewa ruhusa kwenda Barazili kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya Dada yake akarudi akiwa bora na kufanikiwa kufunga katika michezo mitatu iliyofuata.

Na ndipo utani wa Ramos ulipotokea.

 

 

 

Facebook Comments

Related posts