WAHUBIRI WATWANGANA MAKONDE WAKIGOMBEA SADAKA KWENYE BASI

 

Abiria katika gari moja la usafiri wa uma (daladala) walibaki vinywa wazi baada ya wahubiri wawili kutwangana makonde kila mmoja akitaka awahubirie abiria hao na kukusanya sadaka.

Kisa hicho kilitokea katika gari moja la abiria katika eneo la Kiritiri Embu nchini Kenya baada ya muhubiri mmoja kuingia katika gari hilo na kutaka ahubiri hali ya kuwa tayari mwenzake alishaanza kuhubiri abiria hao.

”Sasa mbona unakuja kuhubiri hapa ilhali unaona nishaingia na kuanza kusoma Biblia. Toka nje na uende ukahubiri kwa gari jingine,’’ mmoja alimwambia mwenzake.

‘’ Hakuna yule ambaye ana haki za kipekee kuhubiri kwenye gari hili. Wacha tuhubiri kwanza mazungumzo yaje baadaye,’’ alimjibu.

Kwa hasira , muhubiri huyo alimvamia mwenzake na kumkaba koo kisha kumvurumishia makonde.

Kufuatia hali hiyo dereva wa gari hilo aliegesha gari pembeni na kuwatimua wote wawili.

”Ovyo kabisa, Mbona mwachapana. Hakuna nitakayemruhusu kuhubiri katika gari hili tena,tokeni nje ’’. Dereva huyo alisikika..

Wahubiri hao walilazimika kushuka huku wakivurumishiana matusi huku wakienda zao

Facebook Comments

Related posts