AUWA MTOTO KWA KUMTUPA CHOONI NA KUTOKOMEA

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka arobaini anasakwa na polisi kwa kosa la kumtupa mtoto wake chooni.

Inadaiwa mwanamke huyo aliyeshirikiana na mumewe kabla ya kutenda kisa hicho alimtaarifu daktari kuwa angefanya hivyo muda mchache baada ya kujifungua.

Kisa hicho kimeripotiwa kutokea katika eneo la kijiji cha Kibingo eneo la Kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya.

Mwanamke huyo anadaiwa kutenda kisa hicho na kutokomea.

Awali daktari aliwafahamisha watu kuwa makini mno na mwanamke huyo lakini kwa bahati mbaya, aliutekeleza unyama huo

Visa vya wanawake kuwatupa watoto wao vimekuwapo kwa muda mrefu na vinazidi kuendelea ingawa vyombo husika vimekuwa vikijitahidi kuvidhibiti.

Mnamo Agosti, Msamaria Mwema mjini Thika, alimuokoa mtoto mchanga aliyekuwa ametupwa kichakani.

Katika kisa kingine kilichotokea Oktoba mwaka huu, mama kutoka Kaunti ya Vihiga, alimuacha mwanawe wa miezi minne hospitalini

Facebook Comments

Related posts