Uzembe utamponza bwana mdogo Dembele kushindwa kutakata Catalonia.

Nyota kutoka Uruguay, Luis Suarez amemuonya mchezaji mwenza Ousmane Dembele Kwamba kama anataka kufanikiwa katika Klabu ya Barcelona basi ajifunze kuwa makini.

Wawili hawa wakutana leo katika mchezo wa kirafiki ambapo Uruguay watakuwa wageni wa Mabingwa wa kombe la Dunia Ufaransa pale Stade De France kwanzia saa Tano usiku.

Suarez akizungumzia kuelekea mchezo wa leo akakanusha taarifa kuhusu winga huyu wakifaransa kushindwa kuendana na soka la Barcelona akiishia tu kumpa ushauri bwana mdogo ajirekebishe.

“Sio Kwamba hajaendana na mazingira kwa sababu uhusiano wake na wachezaji wengine ni mzuri, na tunamuona akiwa na Furaha”

“Lakini kama baadhi ya wachezaji wenzangu wanavyosema na Osman anajua, soka ni kama bahati kwa Kila mchezaji na nnafikiri anapaswa kuwa makini na kuwa mwangalifu kwenye baadhi ya maeneo”

Tangu Dembele ajiunge na Barcelona akitokea Borussia Dortmund 2017 kwa day nono la £ milioni 97 ameshindwa kuonyesha samani ya pesa hizo pale Camp Nou.

Taarifa zilizo ripotiwa na jarida la As zilidai Dembele ameshindwa kuhudhuria mazoezi kutokana na kucheza Game na marafiki zake usiku kucha.

Facebook Comments

Related posts