Hata kama kuna Lacazette na Aubameyang, Welbeck awaingiza Arsenal sokoni.

Mkuu wa Kitengo cha Soka ndani ya klabu ya Arsenal Raul Sanllehi amekiri kwamba jeraha kubwa la Danny Welbeck huenda likawalazimisha kubadili mipango yao ya usajili ya mwezi Januari .

Welbeck amefanyiwa upasuaji mara mbili baada ya kuumia kifundo cha mguu kwenye mechi ya Europa dhidi ya Sporting Lisbon.

Huku akiwa na Historia kubwa ya majeraha , huenda maisha ya Welbeck ndani ya Gunners yakiwa yamefika kikomo kutokana na mkataba wake kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu.

Baada ya jeraha la Welbeck , kocha Unai Emery alisema kwamba atampa nafasi mshambuliaji chipukizi Eddie Nketiah  kuziba pengo la Danny.

Huku  Sanllehi akikubaliana na kocha Unai, hakutaka kufunga mlango wazo la kuzama sokoni kufanya usajili lakini pia amesisitiza kwamba Welbeck atapata msaada wa kila aina mpaka kupona.

Facebook Comments

Related posts