ASKARI POLISI AUA KWA KISU AKILINDA MCHEPUKO WAKE

 

Bwana mmoja askari wa polisi amejikuta matatani baada ya kuripotiwa kumuua mtu mmoja kwa kumchoma kisu kutokana na wivu wa mapenzi.

Bwana huyo Robert Otieno Otunga anadaiwa kutenda kisa hicho kwa George Odhiambo Misao mwenye umri wa miaka 37 baada ya kumfumania nyumbani kwa mchepuko wake aitwaye Beatrice Anyango.

Mauaji hayo yalifanyika usiku wa Jumanne, Novemba 20 katika kijiji cha Wiga kaunti ya Homa Bay nchini Kenya.

Hata hivyo inadaiwa kuwa mchepuko huo ni mjane na kuwa ulikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na askari huyo .

Chifu wa eneo hilo Andrew Okach alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku mwili wa marehemu ukipelekwa hospitali ya Homa Bay kwa uchunguzi zaidi.

Facebook Comments

Related posts