AUA MWANAYE KWA MPINI WA JEMBE AKIMTUHUMU KUIBA KUKU.

 

Polisi mkoani Manyara wanamshikilia mwanamke mmoja Mariam Daudi kwa tuhuma za kumuua mwanaye kwa madai ya kuiba njiwa wa jirani.

Mwanamke huyo mkazi wa Komoto wilaya ya Babati mkoani humo anadaiwa kumuua mwanaye Emanuel Justine (11) mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Kwang’w.

Kamanda wa polisi mkoani humo Augustino Senga alisema mwanamke huyo siku ya tukio alipokea taarifa kuwa mwanaye aliiba njiwa za jirani.

Baada ya kupokea taarifa hizo alimkamata mwanaye kwa kushirikiana na anayedaiwa kuiba njiwa kisha kumfunga kamba mikono na miguu kisha kuanza kumcharaza viboko ambapo jirani alitumia fimbo za mbaazi huku mama huyo akitumia mpini kwa madai kuwa amechoshwa na tabia ya mwanaye.

Adhabu iliendelea hadi mtoto huyo alipopoteza maisha.

Polisi wanaendelea na msako ili kumtia nguvuni mwanaume aliyeshirikiana na mama huyo kutoa adhabu hiyo kwa mtoto huyo.

Related posts