Zabaleta amkaribisha kwa Mikono miwili Nasri wawe pamoja tena kwa wagonga nyundo.

Kumpata nyota wa zamani wa Arsenal na Manchester City, Samir Nasri kutasaidia kuongezeza kuongeza nguvu kwenye kikosi cha wagonga nyundo wa London Westham United na hilo ni kwa mujibu wa Pablo Zabaleta.

Mara ya mwisho Nasri kucheza kwenye mechi ya kimashindano ni takribani mwaka mmoja umepita, akiwa anaitumikia Antalyaspor katika ligi kuu ya soka nchini Uturuki, na sasa anajipanga kurejea uwanjani Tangu atoke kwenye kifungo cha matumizi ya Dawa zisizo ruhusiwa michezoni ambapo tayari ameshapata matibabu katika mji wa Los Angeles mwaka 2016 wakati akiwa kwa mkopo Sevilla. 

Adhabu aliyokuwa amepewa kwa taratibu za Uefer alikuwa hapaswi Kufanya kutumikia Klabu yeyote inayotambulika mpaka mwanzoni mwa Mwezi Novemba.

Baada ya hapo Nasri amekuwa akipasha na kikosi cha Westham chini ya mwalimu Manuel Pellegrin na anajipanga kujiunga na mwalimu huyo kwa mara nyingine ambapo walishawahi Kufanya kazi pamoja katika Klabu ya Manchester City.

Mbali na kujiunga tena na Pellegrin, Nasri mwenye uraia wa Ufaransa anatarajia pia kucheza pamoja na beki Zabaleta ambaye pia alicheza nae wakiwa City.

Katika mahujiano na Sky Sports Zabaleta amemwagia sifa Nasri akidai Klabu yao inahitaji kuwa na wachezaji wa kiwango kama cha Nasri.

 

Related posts