AMUUA MKEWE KWA PANGA,NI BAADA YA KUMFUMANIA NA MWANAUME MWINGINE CHUMBANI KWAKE

 

Mwanaume mmoja Paul Maritim ameripotiwa kumuua mkewe kwa kumchinja shingoni kwa panga baada ya kumkuta akifanya mapenzi na mwanaume mwingine chumbani kwao.

Mbali na mauaji hayo pia mwanaume huyo mkazi wa kijiji cha Kapregerego kaunti ya Nakuru nchini Kenya anadaiwa kumjeruhi kwa mapanga mwanaume aliyemfumania na mkewe wakifanya tendo hilo.

Siku ya tukio Maritimu alirejea nyumbani kwake na kumfumania mkewe akiwa na mwanaume chumbani kwake jambo lilimghadhabisha na kuamua kuchukua panga na kuwashambulia.

Majirani waliofika katika eneo la tukio kushuhudia kilichokuwa kikiendelea, inasemekana walifurushwa na Maritim huku akitishia kuwakatakata pia.

Tayari maafisa wa polisi wanamsaka Maritim ambaye alitoweka baada ya kutekeleza kitendo hicho cha Jumatano November 21mwaka huu ili kujibu tuhuma za mauaji ya mkewe bi. Janet Maritim.

Related posts