Mane akubali maisha ya kubaki Anfield mpaka 2023

Sadio Mane amekubaliana na klabu yake ya Liverpool kuhusu kupewa mkataba mpya wa muda mrefu katika klabu hiyo, mkataba ambao utamuweka Anfield mpaka mwaka 2023.

Kocha wa klabu hiyo Jurgen Klopp amemwagia sifa nyota huyo Msenegal akidai “sidhani kama kuna klabu hata moja Ulaya itakataa kuwa na mchezaji kama yeye”.

Mane mwenye umri wa miaka 26 amefunga magoli 40 kwenye michezo 89 aliyoichezea Liverpool tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Southampton kwa dau la paundi milion 34 kwenye majira ya kiangazi mwaka 2016.

Mane akizungumzia mkataba wake mpya “nina furaha kuongeza mkataba mpya ndani ya klabu ya Liverpool”.

 

 

 

 

Related posts