Baada ya kuandamwa na Maneno dogo afikia maamuzi haya, huwezi amini.

Ousmane Dembele ameiomba Klabu Barcelona imruhusu aondeke katika dirisha la usajili Mwezi January taarifa hii inachangiza uvumi kutoka vyanzo mbalimbali vya habari kuhusu kurejea kwa Neymar Camp Nou.

Dembele ameshindwa kuendana na mfumo wa Barcelona tangu ajiunge na Klabu hiyo ya pale Catalunya mwaka 2017 akitokea Borussia Dortmund kwa dau la paundi milion 93 Sawa na Euro milioni 105 na sasa anaomba uongozi wa Barcelona umfungulie mlango aondoke.

Taarifa zinadai Barcelona iliyopo chini ya Kocha Ernesto Valverde inajipanga kumjumuisha Dembele kwenye dili litakalomng’oa Neymar pale Paris nakurejea Catalunya.

Vilabu vya England pia haviko mbali kumfuatilia Dembele mshindi wa kombe la Dunia mwaka 2018 akiwa na Ufaransa ambapo ambapo Vijogoo Liverpool wanahusishwa kuhitaji huduma yake.

Dembele amejikuta njia panda katika maisha yake ya soka Barcelona katika Wiki za hivi karibuni baada ya Jarida la As kuripoti kuwa alikosa mazoezi katika Klabu yake siku moja kutokana na kucheza game na marafiki zake usiku kucha.

 

 

Related posts