Hazard awakatalia mchana kweupe matajiri wa Jiji la Paris wasijisumbue kumtafuta.

Nyota wa klabu ya Chelsea Eden Hazard hakubaliani na mipango ya kuhamia Paris Saint-Germain lakini amekumbushia kwa inawezekana kuhama darajani.

Eden Hazard amekuwa akihusishwa kuhama darajani kitambo ikiwa ni kabla na baada ya kombe la Dunia na kujiunga hasa na Real Madrid.

Hazard mwenyewe alishaonyesha hamu yake ya kutaka kujiunga na matajiri wa jiji la Madrid ( Los Blancos) lakini hata hivyo Chelsea wamekuwa wakipambana kuhakikisha Nyota wao huyo haondoki kizembe.

Enzi zake Hazard akiwa Lile ya Ufaransa kabla ya Kujiunga na Chelsea.

Lakini Hazard akiwa katika mahojiano na wanahabari Hazard alikubali kuhusu taarifa za yeye kuwindwa na Paris Saint-Germain inayoshiriki Ligue 1 ila yeye akaweka wazi kutokuwa na hamu ya kujiunga na Klabu hiyo akisema kama ni kwenda Ufaransa basi labda arudi Lile.

“Kama nitatudi Ufaransa siku moja basi nitakwenda Lile”.

“Lakini kwa sasa hivi hakuna nafasi Kwamba nitarejea kwenye Ligi ya Ufaransa”.

Eden Hazard pia amesisitiza hawezi kuondoka Chelsea kwenye dirisha dogo la Usajili Mwezi January mbali na kuhusishwa na Real Madrid akisema kuna uwezekano wa kuondoka msimu utakapo malizika.

 

Related posts