Hatimaye aliyeshambulia basi la Dortmund kwa bomu mwaka 2017 auhukumiwa miaka 14 Jela.

Hatimaye mtu aliyefanya shambulizi la bomu kwenye basi la kusafiria la Klabu ya Borrusia Dortmund mwaka 2017 amehukumiwa Jela kwa kifungo cha miaka 14 kwa kosa la kujaribu Kufanya mauaji.

Mtu huyo ajulikanaye kifupi kama Sergej W. amekutwa tuhuma hiyo na kuhukumiwa leo na mahakama mjini Dortmund.

Hata hivyo alitakiwa kulipa kiasi cha euro 15000 kwa beki wa Dortmund Marc Bartra ambaye alipata majeraha kwenye shambulio hilo ambaye alitakiwa kufanyiwa upasuaji kutoa vipande vya kioo vilivyo ingia mkononi.

Askari mmoja pia alijeruhiwa katika shambulio hilo ambapo milipuko mitatu ililipukia basi hilo la Dortmund wakati wa safari kutoka Mji wa Magharibi wa Ujerumani Kuelekea kwenye mchezo wao wa nyumbani katika michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Ac Monaco Tarehe1 April 2017.

Related posts