Majeruhi yaiandama City Kocha achagua jembe lake kuimaliza Lyon Leo.

Usiku wa Ulaya, michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya imerejea na ipo katika hatua ya makundi leo jumanne na kesho jumatano pia kuna michezo inapigwa.

Kuelekea michuano hii Kocha wa Manchester City amependekeza kumtumia kinda Phil Foden Kwamba ataanza katika mchezo ambao wataumana na Lyon ya Ufaransa.

City wanaingia katika mchezo wa leo pale katika dimba la Groupama bila ya Nyota wao kadhaa kama Bernado Silva na Ilkay Gundogan.

Bwana mdogo Foden amecheza kwa dakika 3 tu msimu huu kwenye michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya lakini ametokea bechi Mara saba kwenye ligi kuu ya England.

Na Guardiola amesema bwana mdogo anapaswa kucheza katika mchezo wao leo dhidi ya Lyon kule Ufaransa ikiwa ni mchezo wa Kundi F City wakiwa kileleni wakiipita Lyon kwa alama 3.

“Wakati Phil ancheza kwenye mchezo wa mwisho wa Pre- season alinishawishi na sasa ananguvu na yupo tayari kucheza na sisi hakuna tatizo. ¬†Maneno ya Guardiola.

Related posts