BEKI HILI KUTOKA IVORY COAST LATUA RASMI MSIMBAZI.

Klabu ya wekundu wa msimbazi Simba wamethitisha kunasa saini beki wa kushoto kutoka Ivory Coast ajulikanaye kama Zana Coulbaly.

Zana Coulbaly beki wa pembeni

 

Taarifa kupitia ukurasa wa Instagram wa Simba imesomeka “Tunapenda kuwatangazia kwamba beki Zana Coulibaly kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast leo atawasili nchini kwa ajili kukamilisha taratibu za mwisho kujiunga na timu yetu ili kuziba pengo la beki Shomari Kapombe ambaye siku za karibuni alipata majeraha. #SSC #NguvuMoja”

Simba ni Klabu ambayo ina michuano mingi yakushiriki msimu huu ikiwemo michuano ya Klabu bingwa barani Afrika hivyo kinahitajika kikosi kipana cha kuwasaidia kuleta ushindani. 

Related posts