FAINALI YA KLABU BINGWA AMERICA YA KUSINI KUCHEZWA MADRID RAISI (CONMEBOL) AWATAKA MASHABIKI WAJIHESHIMU.

Raisi wa shirikisho la kandanda Amerika ya kusini (CONMEBOL)  Alejandro Domiguez amewataka Mashabiki kujieheshimu Kuelekea fainali ya pili ya (COPA LIBERTADORES) michuano ya Klabu bingwa barani America ya kusini unapangwa kupigwa jijini Madrid.

Boca Juniors na River Plate wataumana katika Uwanja wa Santiago Bernabeu siku ya December 9 kumalizia mechi ya marudiano ambapo mechi ya mwanzo ilimalizika kwa sare ya 2-2.

Mchezo huo awali ulikuwa uchezwe nyumbani kwa River Plate pale El Monumental lakini mechi ikaahirishwa baada ya basi la Boca kuvamiwa njiani likielekea wa uwanjani.

Sasa mchezo huo utachezwa mbele ya Mashabiki wa Boca na Mashabiki wa River katika mchezo ambao utatambulika kama ni wanyumbani kwa River.

Domiguez kwa mara ingine anawaonya mashabiki kwa vitendo vyao lakini anaamini watasherekea vyema mchezo wa Marudiano.

“Spain ni Nchi yenye raia wengi wa Argentina ambao wapo nje ya Nchi Yao, Madrid ni Moja ya majiji 10 yenye muonekano mzuri Duniani na wenye utamaduni wa soka, napenda kila mtu atakae ingia aonyeshe namna ya kufurahia na awe na muda mzuri wa kushangilia.

Bado Klabu ya Boca wanalishishtaki shirikisho la soka (CONMEBOL) kwa maamuzi yake yakutokuwapa wao ubingwa baada ya kuvamiwa.

 

Related posts