ASKARI POLISI AUA KWA KISU AKILINDA MCHEPUKO WAKE

  Bwana mmoja askari wa polisi amejikuta matatani baada ya kuripotiwa kumuua mtu mmoja kwa kumchoma kisu kutokana na wivu wa mapenzi. Bwana huyo Robert Otieno Otunga anadaiwa kutenda kisa hicho kwa George Odhiambo Misao mwenye umri wa miaka 37 baada ya kumfumania nyumbani kwa mchepuko wake aitwaye Beatrice Anyango. Mauaji hayo yalifanyika usiku wa Jumanne, Novemba 20 katika kijiji cha Wiga kaunti ya Homa Bay nchini Kenya. Hata hivyo inadaiwa kuwa mchepuko huo ni mjane na kuwa ulikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na askari huyo . Chifu wa eneo…

Read More

Hata kama kuna Lacazette na Aubameyang, Welbeck awaingiza Arsenal sokoni.

Mkuu wa Kitengo cha Soka ndani ya klabu ya Arsenal Raul Sanllehi amekiri kwamba jeraha kubwa la Danny Welbeck huenda likawalazimisha kubadili mipango yao ya usajili ya mwezi Januari . Welbeck amefanyiwa upasuaji mara mbili baada ya kuumia kifundo cha mguu kwenye mechi ya Europa dhidi ya Sporting Lisbon. Huku akiwa na Historia kubwa ya majeraha , huenda maisha ya Welbeck ndani ya Gunners yakiwa yamefika kikomo kutokana na mkataba wake kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu. Baada ya jeraha la Welbeck , kocha Unai Emery alisema kwamba atampa nafasi…

Read More

AUWA MTOTO KWA KUMTUPA CHOONI NA KUTOKOMEA

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka arobaini anasakwa na polisi kwa kosa la kumtupa mtoto wake chooni. Inadaiwa mwanamke huyo aliyeshirikiana na mumewe kabla ya kutenda kisa hicho alimtaarifu daktari kuwa angefanya hivyo muda mchache baada ya kujifungua. Kisa hicho kimeripotiwa kutokea katika eneo la kijiji cha Kibingo eneo la Kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya. Mwanamke huyo anadaiwa kutenda kisa hicho na kutokomea. Awali daktari aliwafahamisha watu kuwa makini mno na mwanamke huyo lakini kwa bahati mbaya, aliutekeleza unyama huo Visa vya wanawake kuwatupa watoto wao vimekuwapo kwa muda mrefu…

Read More

Uzembe utamponza bwana mdogo Dembele kushindwa kutakata Catalonia.

Nyota kutoka Uruguay, Luis Suarez amemuonya mchezaji mwenza Ousmane Dembele Kwamba kama anataka kufanikiwa katika Klabu ya Barcelona basi ajifunze kuwa makini. Wawili hawa wakutana leo katika mchezo wa kirafiki ambapo Uruguay watakuwa wageni wa Mabingwa wa kombe la Dunia Ufaransa pale Stade De France kwanzia saa Tano usiku. Suarez akizungumzia kuelekea mchezo wa leo akakanusha taarifa kuhusu winga huyu wakifaransa kushindwa kuendana na soka la Barcelona akiishia tu kumpa ushauri bwana mdogo ajirekebishe. “Sio Kwamba hajaendana na mazingira kwa sababu uhusiano wake na wachezaji wengine ni mzuri, na tunamuona…

Read More

ABAKWA NA WANAUME WAWILI NJIANI AKIELEKEA KUJIFUNGUA

  Mwanamke mmoja mjamzito ameripotiwa kubakwa na wanaume wawili mbele ya watoto wake akiwa njian kwenda hospitali kujifungua. Mjamzito huyo kutoka mtaa wa Huruma jijini nairobi siku ya tukio akiwa na mwanaye walikutana na wanaume hao waliowachukua kwa nguvu hadi vichakani na kumbaka bila kujali hali yake mbele ya mwanaye. Wabakaji hao walidaiwa kumtishia mama huyo kumuua endapo atatoa taarifa polisi. Tayari maafisa wa polisi wamefanikiwa kumtambua mmoja wa washukiwa hao wa ubakaji aitwaye Kamau au kwa jina la utani Kamare ambaye anaishi na mjombake katika eneo la Mlango Kubwa…

Read More

APONZWA NA KITABU CHA NGONO ,SASA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA MIAKA KUMI GEREZANI

Mwandishi mmoja wa vitabu nchini Uchina amefungwa miaka 10 jela kwa kuandika na kuuza kitabu chenye maudhui ya ngono ya wapenzi wa jinsia moja. Mwandishi huyo mwanamke afahamikaye kwa jina la Liu, alihukumiwa kifungo hicho na na mahakama ya jimbo la Anhui mwezi uliopita kwa kuuza “maudhui machafu”. Jina la kitabu hicho ni “Occupation”, lenye maana ya kazi kwa kiswahili na kimebeba maudhui ya “tabia ya ngono ya wapenzi wa jinsia noja wa kiume…pamoja na aina za kupotosha za ngono na kwenda kinyume na jamii.” Kwa mujibu wa shirika la…

Read More

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amekiri kuwa alidanganya wabunge

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amekiri kuwa alidanganya wabunge waliokuwa wanachunguza ufisadi serikalini aliposema kuwa dola $35,000 zilizotumwa kwa akaunti yake kutoka kampuni ya Bosasa, zilikuwa ni malipo kwa ushauri wa mwanaye Andile. Hata hivyo uchunguzi umebaini pesa hizo zilikuwa mchango kwa kampeni yake. Malipo hayo yakifanyika punde baada ya Kampuni hiyo kushinda zabuni kubwa ya serikali. Je kampeini ya rais Ramaphosa dhidi ya rushwa na ufisadi imeingia doa?

Read More

MBARONI KWA KULEWESHA WANAUME NA KUWAIBIA

  Polisi nchini Kenya wamefanikiwa kuwatia nguvuni wanawake wawili wauza milii kwa kosa la kuwachaganyia dawa za kulevya wateja wao na kuwaibia. Wanawake hao Mary Nyaguthii Mathari na Mary Nyamwea Gathiaka walikamatwa Ijumaa, Novemba 16, na walipatikana na dawa kadha zinazoaminiwa kutumiwa kuwalevywa wateja wao katika vilabu vya burudani. Mbali na dawa hizo walikamatwa na kadi za simu na za kutolea pesa. “Makechero waliotumia ripoti za kijasusi waliwakamata wanawake wawili; Mary Nyaguthii Mathari na Mary Nyamwea Gathiaka mjini Thika kwa madai ya kuwalevywa wateja wao kabla ya kuwaibia. Tembe kadhaa…

Read More

WAHUBIRI WATWANGANA MAKONDE WAKIGOMBEA SADAKA KWENYE BASI

  Abiria katika gari moja la usafiri wa uma (daladala) walibaki vinywa wazi baada ya wahubiri wawili kutwangana makonde kila mmoja akitaka awahubirie abiria hao na kukusanya sadaka. Kisa hicho kilitokea katika gari moja la abiria katika eneo la Kiritiri Embu nchini Kenya baada ya muhubiri mmoja kuingia katika gari hilo na kutaka ahubiri hali ya kuwa tayari mwenzake alishaanza kuhubiri abiria hao. ”Sasa mbona unakuja kuhubiri hapa ilhali unaona nishaingia na kuanza kusoma Biblia. Toka nje na uende ukahubiri kwa gari jingine,’’ mmoja alimwambia mwenzake. ‘’ Hakuna yule ambaye…

Read More

Neymar wewe na Ramosi kwani mna ugomvi?.

Taarifa zinasema kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Brazili na Klabu ya PSG ya pale Ufaransa Neymar Jr anahitaji beki wa Real Madrid Sergio Ramos aondeke ndipo ajiunge na Klabu hiyo Tajiri wa Jiji la Madrid. Sasa swali ni Kwamba inawezekana Ramos akawa kikwazo cha Neymar Jr kujiunga na Real Madrid ambayo inamuhitaji kwa muda mrefu? Taarifa kutoka Don Balon zinadai mbrazili huyo hayuko tayari kucheza na Nyota huyo kihispania na hata weza kujiunga na Madrid endapo Ramos yupo kwenye timu. Makisio ya Chanzo cha Neymar kutohitaji kucheza na Ramosi timu…

Read More