Cr7 LIGI NYINGINE REKODI NYINGINE, “AVUNJA REKODI YA 1957”.

Huu ni msimu wa kwanza kwenye Serie A, kwa Nyota Christiano Ronaldo tangu ajiunge na Juventus akitokea Real Madrid lakini ameonekana Kufanya vyema mbali na Ugeni wake kwenye Ligi.

Baada ya kuweka kambani Jumamosi kwenye mechi dhidi ya Fiorentina , Cristiano Ronaldo ameweza kufikia rekodi iliyokuwepo tangu mwaka 1957 .

Tangu nyota wa zamani wa kimataifa wa Wales na klabu ya Juventus John Charles kuweza kufunga magoli 10 katika mechi 14 za kwanza hakuna mchezaji mwingine aliyeweza kufanya hivyo mpaka msimu huu CR7 kufanya hivyo.

Na sasa Ronaldo kwenye chati ya ufungaji yupo sawa na Straika wa Genoa, Krzysztof Piatek wote wakiwa wameweka kambani magoli 10.

 

Facebook Comments

Related posts