Kuelekea uchumi wakati na Tanzania ya viwanda Watanzania kunufaika na viwanda 3300

Kuelekea uchumi wakati na Tanzania ya viwanda watanzania wameelezwa kunufaika na viwanda 3300 vilivyosajiliwa hapa nchini.

Hayo yamebainishwa na msemaji wa serikali Hassan Abass wakati akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Mwanza kupitia Radio jembe katika kipindi maalum akifafanua utendaji kazi wa Rais Dr John Pombe Magufuli kwa miaka mitatu madarakani

Amesema mpaka sasa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wameshajisajili katika uanzishwaji wa mradi huo wa viwanda ikiwa kuna viwanda vikubwa ,vya kati na vidogo ambavyo vitaweza kuwanufaisha watanzania katika nyanja mbalimbali hasa ajira

Aidha dr Abass ameeleza kuwa Tanzania ya viwanda si Dar es Salaam pekee bali katika mikoa yote na kuwataka viongozi wa mikoa kutenga sehemu maalum kwaajili ya uwekezaji

Facebook Comments

Related posts