MODRIC KUUA UTAWALA WA MIAKA 10 WA CR7 NA LA PULGA KWENYE Ballon d’Or LEO?

Muda wa kusubiri unaelekea ukingoni sasa na mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or 2018 atawekwa hadharani baadae usiku waleo kwenye hafla itakayofanyika kwenye mji mkuu wa Ufaransa Paris.

Tuzo zenye heshima kubwa katika soka duniani zitatolewa katika vipengele tofauti tofauti kwa wanaume na kwa wanawake .

Watawala wa tuzo ya mchezaji bora wakiume duniani Ballon d’Or ambao ni Lionel Messi na Christiano Ronaldo watakumbwa na upinzani mkali katika kuwania tuzo hiyo kutokana na uwepo wa mchezaji anayepewa nafasi kubwa kuchukua tuzo hiyo Luka Modric ambaye anaonekana kuua utawala nyota hao wawili kwenye soka Duniani.

Mshambuliaji wa Juventus Christiano Ronaldo na wa Barcelona Lionel Messi wote kwa pamoja wameshinda Ballon d’Or mara tano kila mmoja wakiweka rekodi ya kupokezana tangu 2008, lakini mwaka huu wanaonekana kupoteza uwezekano wa utawala wao waliotawala kwa takribani miaka 10 na hiyo ni kutokana na kushindwa kusaidia mataifa yao yaliyotolewa kwenye hatua ya mtoano kwenye kombe la Dunia 2018 huku wakibebwa tu na mafanikio ya vilabu.

Wachezaji watano wanaopewa nafasi ya kushinda Ballon D’or leo.

1) Luka Modric: Kiungo huyu wa Real Madrid na Croatia anaonekana kuongoza katika mbio za kuwania Ballon D’or 2018, akiisaidia Croatia kufika fainali ya kombe la Dunia 2018 pale nchini Urusi na pia akiisadia kwa kiasi kikubwa Real Madrid kushinda Michuano ya Klabu bingwa Barani Ulaya msimu uliopita. vyanzo vingi vimeshamtabiria kuchukua tuzo hiyo huku Lionel Messi na Ronaldo wakiwekwa mbali na yeye, ikumbukwe alimpiku Ronaldo na kuchukua tuzo ya FIFA ya mchezaji bora wa dunia.

2) Cristiano Ronaldo: Kwa sasa yupo Juventus ameisadia Real Madrid kushinda Makombe matatu Mfululizo ya Klabu Bingwa barani Ulaya msimu uliopita kabla ya kuondoka na kujiunga na Juventus. Alifunga magoli 15 kwenye michezo 13 ya Klabu Bingwa Brani Ulaya na kuisaidia Real kubeba ndoo kwa style ya kipekee, Ronaldo kwa sasa yupo sawa na Lionel Messi kwa kuchukua Tuzo hiyo Mara 5 na tuzo yake ya kwanza alichukua mwaka 2008 akiwa na Manchester United kabla ya kuja kushinda Tuzo hiyo Mara 4 akiwa na Real Madrid ikiwa ni miaka ya 2013, 2014, 2016, na 2017.

3) Kylian Mbappe: Bwana mdogo kaonyesha uwezo wa aina yake katika ulimwengu wa soka, Kyilian Mbappe alikuwa katika kiwango cha aina yake katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 akiisadia Ufaransa kuchukua kombe hilo. Aliibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora kinda katika michuano hiyo na yeye pia anapewa nafasi ya kushinda Ballon D’or leo.

 

Facebook Comments

Related posts