KWA MARA YA KWANZA NDANI YA MIAKA 10 MODRIC AWEKA HISTORIA BALLON d’0r.

Luka Modric ameshinda tuzo ya Ballon d’Or 2018 akimpiku Christiano Ronaldo na Antoine Griezman huku Lionel Messi akikamata nafasi ya tano.

Ni mara ya kwanza ndani ya miaka 10 kumkosa Ronaldo na Messi katika kuchukua tuzo hii yenye heshima kubwa katika soka inayotolewa na chama cha soka pale nchini Ufaransa.

Harry Kane ni muingereza pekee kwenye orodha fupi ya wachezaji 30 bora wa Ballon d’Or akishika nafasi ya 10 baada ya kuchukua tuzo ya ufungaji bora katika michuano ya kombe la dunia 2018.

Mwaka 2018 , Modric alishinda kombe la klabu bingwa ulaya kwa mara ya tatu mfululizo akiwa na klabu yake ya Real Madrid na pia aliisadia Croatia kufika fainali yao ya kwanza kwenye kombe la dunia wakipoteza mbele ya France kwa goli 4-2.

Wachezaji wengine watatu wa Premier League wameingia kumi bora ambao ni Mohamed Salah nafasi ya (6), Eden Hazard (8) na Kevin De Bruyne (9).

 

Facebook Comments

Related posts