MCHUNGAJI ASHAMBULIWA KWA MAWE AKITUHUMIWA KWA UCHAWI MKOANI KATAVI

Wananchi wakiwemo Waumini wavamia nyumba ya Mchungaji wa Kanisa la Sauti ya Uzima, Elia Zabron Balashika(36) maarufu ‘Nabii Elia’ raia wa Burundi na kuishambulia kwa mawe

Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Damas Nyanda alisema tukio hilo lilitokea Mtaa wa Kazima Ringini Manispaa ya Mpanda ambapo Mchungaji huyo amekuwa akitoa huduma kwa miaka sita katika eneo hilo

Chanzo ni imani za ushirikina baada ya taarifa kuzagaa kuwa Nabia Elia aliweka ‘misukule’ watano nyumbani kwake ambao waumini wa kanisa walimtaka awatoe hadharani

Taarifa zilitolewa Polisi ambapo walifika eneo la tukio na kuanza kuwatawanya Wananchi hao lakini ndugu wawili wa Mchungaji Elia, Mussa Elia(24) na Joseph Elia(29) walijeruhiwa kwa kupigwa na mawe kichwani

Aidha, mali za Nabii Elia zilizoharibiwa ni pamoja na vioo vinne vya madirisha ya nyumba yake, kioo cha nyuma cha gari lake la Spacio huku thamani kamili haijafamika

Related posts