SOUTHAMPTON YAMPATA KOCHA MPYA MWENYE UZOEFU NA SOKA LA UJERUMANI.

Ralph Hasenhuttl amechaguliwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Southampton amayo kwa sasa ipo kwenye hali mbaya katika ligi kuu soka nchini England na amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu.

Kocha huyo wa zamani wa RB Leipzig anachukua mikoba ya Mark Hughes ambaye alitimuliwa siku ya jumatatu akiiacha klabu hiyo ya watakatifu ikiwa nafasi ya 18 kwenye msimamo.

Mbali na kuifudisha RB Leipzig, kocha Hasenhuttl amewahi kuvifundisha vilabu vya SpVgg Unterhaching na Ingolstadt.

Facebook Comments

Related posts