GOMEZ AFATA MKUMBO WA KINA SALAH NA MANE KATIKA HILI.

Baada ya kushuhudia siku kadhaa zilizopita mastaa wa klabu ya vijogoo wa jiji Liverpool wakiongeza mkataba kusalia kwenye klabu hiyo leo Joe Gomez kaongeza mkataba wa kusalia klabu hiyo kwa miaka mitano na nusu. Joe Gomez ambaye ni beki sasa atabaki Liverpool mpaka mwaka 2024. Gomez anaungana na mastar wengine kama Bob Firminho, Mo Salah na Sadio Mane ambao tayari washaongeza mikataba ya miaka mitano kila mmoja kusalia Anfield. Facebook Comments

Facebook Comments

Read More