BARCELONA INAWEZA “KUMUIBA” KANE, KAMA ILIVYOTOKEA KWA RONALDO.

Christiano Ronaldo alichukuliwa toka ligi kuu ya soka nchini England na kuhamishiwa La Liga ya pale Spain sasa kocha Maurcio Pochettino anawaza hilo pia huwenda likatokea kwa Harry Kane.

Maurcio Pochettino ansema Barcelona ama klabu nyingine itamuiba Harry Kane kutoka Tottenham.

Kane amekuwa akiwindwa na Barcelona kwa kipindi kirefu huku klabu hiyo ikitafuta mchezaji atakaye kuwa mbadala wa muda mrefu wa Luis Suarez ambaye umri unamtupa mkono.

Kocha wa Barcelona Ernesto Valverde amemzungumzia Kane kama mchezaji hatari kuelekea game yao leo katika michuano ya klabu bingwa Barani Ulaya mchezo utakao pigwa pale Camp Nou.

Kane tayari ameonesha kwa mbali nia ya kuachana na Tottenham lakini Maurcio Pochettino kocha wake anajua namna mastar wa Ligi kuu ya soka nchini England wanavyojaribiwaga na vilabu vya Spain.

“Imeshatokea kipindi cha nyuma Real Maurcio ikimnasa Christiano Ronaldo toka Manchester United, Coutinho akibebwa toka Liverpool imekuwa ikitokea kwa njia tofauti naamini itatokea pia kwa baada”.

 

 

 

Facebook Comments

Related posts