HOSPITALI YA BUGANDO KUPIMA WENYE SARATANI YA MATITI BURE.

Takwimu zinaonyesha kati ya wanawake laki moja ,wanawake 20 wanapata saratani ya matiti huku 20 kati ya wanawake hao wanafariki kutokana na ugonjwa huo

Kwa kuliona hilo Hospitali ya Rufaa ya Bugando leo wanaanza kutoa huduma ya upimaji na upasuaji kwa wanawake wenye matatizo ya saratani ya matiti kwanzia hii leo mpaka tarehe 14 mwezi huu

Hayo yameelezwa na Daktari bingwa wa upasuaji kutoka hospitali hiyo Dr Vihar Kotecha wakati akizungumza na jembe habari

Ameeleza lengo la utoaji huduma hiyo wanawake wapate fursa ya kujua afya zao juu ya tatizo la kansa ya matiti kupewa ushauri na tiba kabla ugonjwa huo hujafika hatua ya mgonjwa kupoteza maisha

Dr Vihar ameeleza kansa ya matiti inatibika kama mgonjwa akigundulika mapema na kupewa tiba ya ugonjwa huo

Facebook Comments

Related posts