AMSHITAKI BABA YAKE KWA KUTOMJENGEA CHOO

Msichana wa miaka saba nchini India amemshitaki baba yake polisi baada ya kushindwa kutekeleza ahadi aliyomuahidi.

Hanifa Zaara amewaambia polisi kuwa baba yake amekua akimdanganya na kuwataka akamatwe na kushtakiwa.

Msichana huyo amesema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya baba yake kushindwa kutimiza ahadi ya kumjengea choo na kwamba amekuwa akiona aibu kwenda haja vichakani kwa kukosa choo.

Hanifa ambaye anaishi na wazazi wake katika mji wa Ambur, jimboni Tamil Nadu, anasema hajawahi kuona choo nyumbani kwao huku katika mtaa anaoishi ni majirani wachache tu ndio wana vyoo majumbani mwao ambao hata hivyo hawavitumii na badala yake kujisaidia nje.

Wahindi wengi nchini humo hawana vyoo na takribani watu milioni 500 hujisaidia nje hii ni kwa mujibu wa shirika la Unicef.

Katika barua aliyoiandika anasema alipata hamasa ya kuwa na choo nyumbani kwao baada ya kujifunza shuleni madhara ya kiafya ya kujisaidia nje huku akiwataka polisi wamlazimishe baba yake kusaini barua itakayoeleza lini atajenga choo hicho.

Polisi waliamua kumpigia simu baba mzazi wa binti huyo ambae aliharakisha polisi akidhani familia yake ipo kwenye matatizoni na baada ya kufika polisi alipigwa na butwaa kujua sababu ya kuitwa kwake.

Baba yake Ehsanullah amesema alishaanza kujenga choo hicho lakini kwa sasa hana pesa ya kukikamilisha kutokana na kukosa ajir

Kilio cha Hanifa kiliungwa mkono na polisi ambao pia waliwashirikisha viongozi wa wilaya ambao sasa wanachangisha pesa za kujenga vyoo 500 kwenye eneo ambalo anaishi binti huyo.

 

Related posts