HIKI NDICHO KISA CHA KUMWAMBIA MWENYEKITI WA KLABU ANAOGOPA.

Taarifa zinaendelea kumuhusisha kocha wa Tottenham kujiunga na vilabu vya Manchester United na Real Madrid.

Maurcio Pochettino alikuwa katika hali nzuri wakati akizungumzia mustakabali wake katika klabu ya Tottenham siku ya Alhamis na kumtania mwenyekiti wa klabu Daniel Levy akimwambia “anaogopa”, kwamba ataondoka.

Pochettino ameisaidia sana Spurs ikifanikiwa kwenda 16 bora michuano ya Klabu bingwa Barani Ulaya na mpaka sasa klabu ikishika nafasi ya tatu kwenye Premier League.

Manchester United na Real Madrid inasemekana waliingia katika vita ya kumuwania Pochettino lakini kocha huyo mwenye miaka 46 alisaini mkataba wa muda mrefu mwezi May.

Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wao wa nyumbani dhidi ya Burnley jumamosi, akiwaambia mwenyekiti wa klabu anajiskia uwoga kuhusu taarifa za yeye kuhusishwa na Vilabu vingine.

 

Related posts