HIKI NDIO SIRI NZITO KUHUSU MWENENDO MBOVU WA MANCHESTER UNITED.

Sio siri kwamba kwa sasa Mashetani Wekundu kwa sasa wanahaha kuingia katika Kinyang’anyiro cha kuingia katika vilabu vinavyopambania ubingwa kwa sasa pale England lakini kinachowakwamisha ni makundi uwepo wa makundi kambini na hilo ni kwa mujibu wa Tim Sherwood.

Mpaka sasa United wameruhusu magoli 26 kwenye michezo 16 ya Premier League na pia wakikosa nafasi ya kumaliza vinara katika kundi lao kwenye michuano ya Uefa champions League baada ya kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Valencia.

Tim Sherwood ambaye ni kocha na mchezaji wa zamani wa Tottenham amesema United inawachezaji wenye kiwango cha juu duniani kama Paul Pogba, Lukaku, Mata, na De gea lakini wako kwa makundi.

Sherwood anasema mbali na United kuwa na wachezaji wazuri lakini Kocha wao Morihno ana kibarua cha kuwaonganisha wachezaji hadi viongozi ambao kila mtu yuko njia yake.

 

Related posts