HAIJALISHI ANAKIWANGO KIZURI NAMNA GANI KWA HILI RONALDO ATAKAA NJEE TU.

Christiano Ronaldo tayari ameyazoea maisha ya Juve Mapema sana tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Spain lakini kocha Massimiliano Allegri anajipanga kumpa mapumziko Nyota huyo mwenye umri wa miaka 33.

Kocha wa Juventus, Allegri amemwelezea Christiano Ronaldo kama “mchezaji hatari” lakini amepanga kumpumzisha Nyota huyo aliyeifungia Juve goli pekee la ushindi dhidi ya Torino Jumamosi.

Ronaldo aliibuka shujaa katika Dabi  hiyo ya Turin (Derby della Mole) ambapo mshindi huyo mara 5 wa Ballon d’Or aliifungia Juve goli la 5000 kwenye Serie A katika ushindi huo wa ugenini.

Kwenye dakika ya 70 Ronaldo alipachika wavuni mpira wa penati na kumfanya afikishe magoli 11 kwenye ligi msimu huu na kuifanya Juve ikae kileleni kwa utofauti wa alama 11.

Ronaldo ameonekana kufiti kwenye mapema kwenye klabu ya Juve tangu ajiunge nao akitokea Real Madrid lakini hakwamishi mawazo ya kocha Massimiliano Allegri kutaka kumpumzisha.

“Nilishamwambia kwamba atakosa moja kati ya michezo inayofuata kati ya Roma, Atlanta,  au Sampdoria.

 

Related posts