EDEN HAZARD AWEKA WAZI MSIMAMO WAKE PALE DARAJANI KWA SASA ITABIDI WAMUELEWE TU.

Nyota wa klabu ya Chelsea Eden Hazard amesisitiza kwamba kwa sasa analenga zaidi kuipatia klabu yake ushindi kuliko kufikia mafanikio binafsi.

Mbeligiji huyo alimtengenezea Pedro goli kabla ya kufunga mwenyewe wakati Chelsea wakiicharaza Brighton 2-1 katika dimba la Amex siku ya Jumapili kwenye ligi kuu ya soka nchini England.

Hazard kwa sasa amehusika katika magoli 17 ya ligi kwa kufunga na kutengeneza katika mechi 16 za ligi kuu msimu huu tofauti na alivyofanya msimu uliopita.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa sasa ana magoli 98 katika klabu ya Chelsea kihistoria lakini ana msimamo wake kwamba haangalii mafanikio binafsi.

Hazard akiongelea kufikisha magoli hayo amesema “najua yakaribia 100 lakini hilo halipo akilini kwanza, ninacho hitaji ni klabu kushinda ndicho cha muhimu.

WACHEZAJI WANAOONGOZA KWA MAGOLI KATIKA HISTORIA YA KLABU YA CHELSEA 

  1. Frank Lampard magoli 211.
  2. Bobby Tambling magoli 202.
  3. Kerry Dixon magoli 193.
  4. Didier Drogba magoli 164.
  5. Rob Bentley magoli 150.
  6. Peter Osgood magoli 150.
  7. Jimmy Greaves magoli 132.
  8. George Mills magoli 125.
  9. George Hildson magoli 108.
  10. Eden Hazard magoli 98.

Related posts