UJUMBE WA GUARDIOLA BAADA YA MOURIHNO KUTIMULIWA UNITED.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameonesha kuwa kitu kimoja na Jose Mourihno baada ya kocha huyo mreno kufungashiwa virago na klabu ya Manchester United.

Makocha hao wawili walikuwa wapinzani wakutisha kipindi wanaviwakilisha vilabu vya kutoka Spain Barcelona na Real Madrid kwa takribani miaka mitatu, na dhana hiyo watu wakajua itakuwa pale England baada ya Mourihno kuchaguliwa kuwa kocha wa Manchester United muda mfupi tu baada ya Guardiola kujiunga na City mwaka 2016.

Lakini Makocha hao wapinzani wakaangukia katika Urafiki kipindi cha utendaji kazi wao kwenye Premier League na Guardiola anasema ana matumaini Mourihno atarudi kibaruani muda si mrefu.

“niko upande wake” Guardiola akiwa katika mkutano na wanahabari “kama makocha tuko wapweke, wanatutafuta wakijaribu kushinda na pale ambapo haushindi najua kipi kinatokea.

” Kila mara nasema nipo katika nafasi ya Meneja na ni najua fika namna wanavyo hisi na kila mara niko pale kwa sababu tunajihisi wapweke, kila hali nzito ipo kwenye mabega yetu.

 

Related posts