UKWELI KUHUSU OZIL KUKAA BENCHI ARSENAL IKIPIGWA GOLI 2-0 NA TOTTENHAM HUU HAPA.

Kocha wa klabu ya washika mitutu wa London Arsenal Unai Emery ametoa sababu za kuto mjumuisha kikosini Mesut Ozil kwenye mechi ya jumatano usiku wakicheza na Tottenham kwamba ni swala la kiufundi lakini akakataa kujibia swala la mustakabali wa Nyota huyo katika klabu hiyo.

Ozil hakuwa hata kwenye bechi kwenye mchezo huo wa robo fainali ya Carabao Cup ambao Arsenal alipigwa goli 2-0 na Tottenham huku Emery akijitetea kwamba alijua atapata matokeo mazuri kwa kikosi alichokiweka chenye vijana kama Joe Willock na Eddie Nketiah.

“Yalikuwa ni maamuzi ya kiufundi” Unai Emery akiwa kwenye mkutano na Wanahabari “Tulijua wachezaji ambao walikuwa na sisi leo wanafaa kwa mechi hii ya leo.

Lakini Unai Emery akagoma kujieleza kwa nini hakumuita Ozil kikosini au uwezekano wa kumuachia Ozil katika dirisha la usajili mwezi januari.

” Nafikiria kuhusu mechi ya Jumamosi (dhidi ya Burnley) na sio kuhusu maswala mengine” alisema “Nafikiria kuhusu wachezaji wote tunawachezaji 24, 25.

Related posts