SOLSKJAER AJA NA MFUMO HUU WA KIBABU FERG KUWANYOOSHA WAPINZANI WAKE.

Kocha wa muda wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameweka wazi kwamba ameshachukua ushauri toka kwa Sir Alex Ferguson tangu amechukua kibarua cha kuifundisha United kama kocha wa muda.

Solskjaer ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Manchester United alishawahi pewa nafasi na Ferguson katika benchi la ufundi 2007 wakati anastaafu soka.

“alinishawishi kwa kila kitu” maneno ya Solskjaer katika mkutano wake wa kwanza na Wanahabari akielekea kuumana na Cardiff siku ya Jumamosi.

Solskjaer anajipanga kutumia kipindi chote cha maisha yake aliyojfunza mfumo wa Ferguson kukumbusha tena kikosi kucheza “bila ya uwoga”

Related posts