AMSHITAKI BABA YAKE KWA KUTOMJENGEA CHOO

Msichana wa miaka saba nchini India amemshitaki baba yake polisi baada ya kushindwa kutekeleza ahadi aliyomuahidi. Hanifa Zaara amewaambia polisi kuwa baba yake amekua akimdanganya na kuwataka akamatwe na kushtakiwa. Msichana huyo amesema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya baba yake kushindwa kutimiza ahadi ya kumjengea choo na kwamba amekuwa akiona aibu kwenda haja vichakani kwa kukosa choo. Hanifa ambaye anaishi na wazazi wake katika mji wa Ambur, jimboni Tamil Nadu, anasema hajawahi kuona choo nyumbani kwao huku katika mtaa anaoishi ni majirani wachache tu ndio wana vyoo majumbani mwao…

Read More

TRENI YA MWENDOKASI YAPINDUKA, BADO HAIJAFAHAMIKA WALIODHURIKA

Ajali iliyotokea katika eneo la Ankara imehusisha treni ya mwendokasi iliyokuwa inaelekea katika ya mji wa Konya baada ya kugonga kiberenge kilichokuwa kinafanya uchunguzi – Ajali hiyo imetokea katika kituo cha treni Wilayani Yenimahalle baada ya treni ya mwendokasi kushindwa kumimama, hata hivyo uchunguzi zaidi unaendelea kujua chanzo cha treni hiyo kushindwa kusimama – Gavana wa Ankara, Vasip Sahin amesema utaratibu za uokoaji bado zinaendelea lakini bado haijafahamika treni hiyo ilikuwa ikisafiri kwa mwendokasi gani – Mwezi Julai, watu 10 walifariki na zaidi ya 70 kujeruhiwa baada ya treni ya…

Read More

SABABU ZA ISCO KUSUSIA KITAMBAA CHA UNAHODHA HIZI HAPA.

Isco alikataa kitambaa cha unahodha wakutosha Marcelo anatolewa kwenda bechi katika mchezo ambao Real Madrid walishangazwa baada ya kucharazwa nyumbani na CSKA Moscow katika michuano ya Uefa champions ligi. “Sijawasiliana kwa nn Isco alikataa kitambaa cha Unahodha” maneno ya Marcelo. “Nilijaribu kunipatia kitambaa cha unahodha wakati naenda bechi kumpisha Carvajal lakini alikataa” Marcelo beki wa pembeni ambaye alishuhudia klabu yake ikipigwa goli 3-0, anasema badala ya kukubali kitambaa Isco akamwambia mvalishe Carvajal na hakujua sababu ilikuwa ni Nilijaribu.    

Read More

RAISI MAGUFULI ASAINI MKATABA MPYA WA KUFUA UMEME

Rais John Pombe Magufuli leo decemba 12 anasaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa kufua umeme na maji katika Mto Rufiki kwa kushirikiana na nchi ya Misri ikulu jiji Dar es Salaam Rais Magufuli Ameeleza mradi utakapokamilika utaleta faida ya kuwa na umeme wa uhakika nchini na kuchochea sera ya Tanzania ya viwanda Rais Magufuli amefafanua Mradi huo pia utaleta chachu ya utunzaji mazingira hasa kuepuka matumizi ya kukata miti ovyo , kutumia kuni na mkaa nakuanza kutumia umeme katika shughuli mbalimbali Aidha Rais Magufuli ameeleza Katika kipindi cha miaka…

Read More

HOSPITALI YA BUGANDO KUPIMA WENYE SARATANI YA MATITI BURE.

Takwimu zinaonyesha kati ya wanawake laki moja ,wanawake 20 wanapata saratani ya matiti huku 20 kati ya wanawake hao wanafariki kutokana na ugonjwa huo Kwa kuliona hilo Hospitali ya Rufaa ya Bugando leo wanaanza kutoa huduma ya upimaji na upasuaji kwa wanawake wenye matatizo ya saratani ya matiti kwanzia hii leo mpaka tarehe 14 mwezi huu Hayo yameelezwa na Daktari bingwa wa upasuaji kutoka hospitali hiyo Dr Vihar Kotecha wakati akizungumza na jembe habari Ameeleza lengo la utoaji huduma hiyo wanawake wapate fursa ya kujua afya zao juu ya tatizo…

Read More

BARCELONA INAWEZA “KUMUIBA” KANE, KAMA ILIVYOTOKEA KWA RONALDO.

Christiano Ronaldo alichukuliwa toka ligi kuu ya soka nchini England na kuhamishiwa La Liga ya pale Spain sasa kocha Maurcio Pochettino anawaza hilo pia huwenda likatokea kwa Harry Kane. Maurcio Pochettino ansema Barcelona ama klabu nyingine itamuiba Harry Kane kutoka Tottenham. Kane amekuwa akiwindwa na Barcelona kwa kipindi kirefu huku klabu hiyo ikitafuta mchezaji atakaye kuwa mbadala wa muda mrefu wa Luis Suarez ambaye umri unamtupa mkono. Kocha wa Barcelona Ernesto Valverde amemzungumzia Kane kama mchezaji hatari kuelekea game yao leo katika michuano ya klabu bingwa Barani Ulaya mchezo utakao…

Read More

GOMEZ AFATA MKUMBO WA KINA SALAH NA MANE KATIKA HILI.

Baada ya kushuhudia siku kadhaa zilizopita mastaa wa klabu ya vijogoo wa jiji Liverpool wakiongeza mkataba kusalia kwenye klabu hiyo leo Joe Gomez kaongeza mkataba wa kusalia klabu hiyo kwa miaka mitano na nusu. Joe Gomez ambaye ni beki sasa atabaki Liverpool mpaka mwaka 2024. Gomez anaungana na mastar wengine kama Bob Firminho, Mo Salah na Sadio Mane ambao tayari washaongeza mikataba ya miaka mitano kila mmoja kusalia Anfield.

Read More

UNAI EMERY AMWAGIA SIFA DE GEA KUIKOA UNITED NA KIPIGO.

Kocha wa klabu ya Arsenal Unai Emery ameweka wazi kwamba kikosi chake kilikosa furaha kushindwa kuifunga Manchester United kwenye Premier League siku ya jumatano usiku. Huwenda ungekuwa ushindi wa kwanza pale Old Trafford tangu mwaka 2006 kwa klabu ya The gunners lakini goli la Jesse Lingard likaifanikisha Man U kupata sare nyumbani. ”kwenye kipind cha pili, wachezaji wetu walicheza kutafuta ushindi, na nnafikiri tulikuwa karibu kupata goli la tatu lakini De Gea aliokoa mara mbili au tatu michomo ya maana”      

Read More

SOUTHAMPTON YAMPATA KOCHA MPYA MWENYE UZOEFU NA SOKA LA UJERUMANI.

Ralph Hasenhuttl amechaguliwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Southampton amayo kwa sasa ipo kwenye hali mbaya katika ligi kuu soka nchini England na amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu. Kocha huyo wa zamani wa RB Leipzig anachukua mikoba ya Mark Hughes ambaye alitimuliwa siku ya jumatatu akiiacha klabu hiyo ya watakatifu ikiwa nafasi ya 18 kwenye msimamo. Mbali na kuifudisha RB Leipzig, kocha Hasenhuttl amewahi kuvifundisha vilabu vya SpVgg Unterhaching na Ingolstadt.

Read More

MCHUNGAJI ASHAMBULIWA KWA MAWE AKITUHUMIWA KWA UCHAWI MKOANI KATAVI

Wananchi wakiwemo Waumini wavamia nyumba ya Mchungaji wa Kanisa la Sauti ya Uzima, Elia Zabron Balashika(36) maarufu ‘Nabii Elia’ raia wa Burundi na kuishambulia kwa mawe – Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Damas Nyanda alisema tukio hilo lilitokea Mtaa wa Kazima Ringini Manispaa ya Mpanda ambapo Mchungaji huyo amekuwa akitoa huduma kwa miaka sita katika eneo hilo – Chanzo ni imani za ushirikina baada ya taarifa kuzagaa kuwa Nabia Elia aliweka ‘misukule’ watano nyumbani kwake ambao waumini wa kanisa walimtaka awatoe hadharani – Taarifa zilitolewa Polisi ambapo walifika eneo la…

Read More