MCHUNGAJI afikishwa Mahakamani kwa Kumpiga Jirani yake, Kisa…. Ni MKE !!!

KATIKA eneo la NJIRU ambalo lipo katika Jiji la Nairobi Nchini Kenya, Mchungaji Peter Omondi Obama (42) amefikishwa mahakamani na Jirani yake kwa madai ya kumshushia kipigo kwa kitendo cha kumualika Mke wa Mchungaji huyo nyumbani kwake kwa ajili ya “kula Bata”

Kwa mujibu wa mashtaka ambayo yamefunguliwa na Peter Otieno Maloa ambaye ndiye muathirika wa kipigo hicho, inadaiwa kuwa yeye alimualika Mke wa Mchungaji Obama katika nyumba yake ambayo ni jarani na Mtumishi huyo wa Mungu kwa ajili ya Chakula cha jioni, lakini baada ya muda, Mchungaji Obama alifika kwa Bw. Maloa na kuanza kushusha kipigo kwa jamaa huyo pasipo kuuliza ni kitu gani kilikuwa kinaendelea

Aidha jeshi la Polisi katika eneo hilo la Njiru wametoa ufafanuzi kuwa , Mchungaji Obama baada ya kuhojiwa kwa umakini, alitoa ufafanuzi kuwa siku ambayo mke wake alienda kuenjoy kwa jirani yake huyo ambaye wanaishi jirani kabisa, yeye alikuwa amemuachia maagizo Mke wake kuwa apike kitoweo cha “Kuku” pamoja na vyakula vingine ili atakaporudi kutoka katika “mishe” zake apate chakula kizuri.

Lakini baada ya kufika Nyumbani, alikuta kuku yule akiungua, huku mke wake hayupo. Baada ya kumtafuta kwa muda, alibaini kuwa yupo nyumbani kwa jirani yake. Baada ya kuingia ndani kwa Bw. Maloa, alishangaa kumkuta mke wake na jirani huyo wakifurahia Chakula cha jioni huku wakitizama “movie” jambo ambalo lilimkera sana Mchungaji huyo

Baada ya kuona hilo, Mchungaji Obama alianza kulalamika na kufoka, lakini Mke Wake wala hakujitikisa au kuchukua hatua yoyote ya kuondoka katika Nyumba ya Bw. Maloa, hali ambayo iliashiria kuwa ni dharau kwa mume mwenyewe. Bw. Maloa alichukua jukumu la kuanza kumtetea Mke wa Mchungaji Obama, na ndipo Mtumishi huyo wa Mungu alichukua jukumu la kumpiga teke “matata” Bw. Maloa na kuanguka Chini, na baada ya ugomvi kuwa mkubwa, majirani walifika kwa ajili ya kutoa msaada kisha kumpeleka Bw. Maloa Hospitali kwa ajili ya Matibabu.

Baada ya kukamatwa, Mchungaji Obama alikana mashtaka hayo na kuachiwa kwa dhamana ya Kshs 100,000

 

Related posts