50 CENT : “TEAIRRA MARI Nilipe Pesa zangu ndani ya Muda Husika, bila hivyo tutaonana wabaya !!!”

KAMA uakuwa ni Mfuatiliaji mzuri sana katika masuala ya Burudani, tunaamini utakuwa umeshafahamu kuwa Rapper 50 Cents alishinda kesi yake dhidi ya Bibie Teairra Mari ambaye pia ni msanii kutoka Nchini marekani, kwa kile kilichodaiwa kuwa, Teairra Mari alifungua Mashtaka dhidi ya 50 Cents  kuwa yeye ndiye kahusika na uvujishwaji ya clip zake za “ngono”

Mahakama ilifutilia mbali mashtaka hayo yaliyofunguliwa na Teairra Mari ambaye ni hit maker wa mkwaju wa “SPONSOR” na kuamuru kuwa amlipe Rapper huyo ambaye jina lake halisi ni Jackson Curtis kiasi cha USD 30,000 sawa na Takribani Tshs 68,100,000.

Baada ya Mahakama ya Los Angels kutoa maamuzi hayo, 50 Cents ambaye hivi sasa amepewa jina la “Mfalme wa Michambo” kutokana na vitendo vyake vya kurusha madongo kwa watu mbali mbali, ametuma salamu za tahadhari kwa Teiaira Mari kuwa anatakiwa azingatie maamuzi ya mahakama na muda wa kumlipa pesa zake hizo maana hatoacha kumpigia simu kumlipa pesa zake.

50 Cents ambaye ni Hit Maker wa Track ya “Amusement Park” ameliweka wazi kupitia instagram account yake kuwa, afanye afanyavyo ikibidi hata kumuomba pesa hiyo boyfriend wake ili alipe deni lake.

Pia akajazia kuwa, asipofanya hivyo, ataenda kwa uongozi wa kipindi cha TV cha LOVE& HIPHOP ambacho Teairra huwa anafanya kazi hivi sasa ili malipo ambayo anayapata, yaingie kwenye akaunti ya 50 Cents moja kwa moja

#ChukuHii

TEAIRRA MARI atatakiwa kulipa kiasi hicho cha Fedha kwa 50 Cent baada ya mahakama kuona mashtaka ya Bibie huyo dhidi ya 50 Cents hayana mashiko na hakuna ukweli wowote. Kwa mantiki hiyo, Teirra atamlipa 50 Cents gharama za usumbufu 

 

Related posts