WILLY PAUL : “Ninamshukuru Mungu nimepona katika Shambulizi la Kigaidi la DUSIT HOTEL”

NCHI ya Kenya ambayo ni Mshirika wa Ukanda wa Afrika Mashariki bado ipo katika majonzi kwa kupoteza ndugu, jamaa na marafiki sambamba na kupata majeruhi kutokana na shambulio linaloaminika kuwa ni la KIGAIDI ambalo limetokea katika Hoteli ya DUSIT D2 jijini Nairobi.

Wasanii mbali mbali kutoka mataifa mbali mbali ambao wameguswa na tukio hilo kwa namna moja au nyingine, wanazidi kutoa salamu za pole kwa Raia wa Kenya ambao wameathirika kwa asilimia kubwa na tukio hilo, huku wakizidi kupeleka maombi yao kwa Mwenyezi Mungu ili azidi kuwapa Nguvu Wananchi na Serikali ya Kenya kiujumla.

Tukijikita zaidi Nchini Kenya, WILLY PAUL ambaye ni msanii wa muziki wa Injili Nchini humo, ni mmoja kati ya watu waliotoka Salama katika shambulio hilo la kigaidi na hiyo ni kwa mujibu wake yeye mwenyewe kupitia instagram account yake.

Willy Paul ambaye anafanya vema na Track ya “DIGIRII” kwa hivi sasa, alipost kipande cha Video ambacho kinaonesha Wananchi wakikimbia kutoka eneo la tukio na kudai kuwa, anamshukuru Mungu kwa kutoka salama katika shambulio hilo na haamini kama ametoka hai

Katika Post yake, Willy Paul anadai kuwa alikuwa katika Kikao chake kilichokuwa na lengo la kujenga sanaa yake zaidi, akiwa ndani ya Jengo hilo, awali aliskia mlipuko ambao hajawahi kuusikia katika maisha yake. Lakini baadaye alianza kusiki milio ya Risasi, hali ambayo ilimfanya aanze kufanya utaratibu wa kuokoa maisha yake Kadri awezavyo.

Pia ameongeza kuwa, hiyo ni mara yake ya kwanza kukutana na hali ile tangu azaliwe. Lakini ameishi serikali ya Kenya ifanye uchunguzi zaidi kwa hicho kilichotokea, tena kwa kina sana.

Related posts